![]() |
| Mwanamke akikimbia kutafuta hifadhi baada ya mapigano kuzuka katika wilaya ya Miskin, katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui. |
Watu sabini wameuawa katika awamu mpya ya makabiliano na
ghasi zinazoendelea kuitikisa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kamishna wa Pilisi nchini humo, Elie Mbailao, amesema
leo kuwa ghasia hizo mbaya zimetokea katika mji wa Boda, kilometa 100 (maili
62) magharibi mwa mji mkuu, Bangui.
Kwa mujibu wa Kamanda Mbailao, mapigano hayo yaliyogeuka
kuwa ghasia za kidini, yameshuhudia nyumba 30 kuchomwa moto katika mji huo.
Mapigano hayo yanatokea huku kukiwa na vikosi vya
kulinda amani kutoka Ufaransa na vile
vya Umoja wa Afrika, lakini vikosi hivyo vimeshindwa kurejesha amani na usalama
kwa wananchi wanaoteseka. Pia vikosi hivyo vimelaumiwa kushindwa kuzuia mashambulizi
ya kidini nchini humo.
Mapigano hayo ya kidini yamesababisha vifo vya zaidi ya
watu 1,000 ndani ya mwezi Januari na kulazimisha watu zaidi ya milioni moja
kuyakimbia makazi yao na mashamba yao.

0 comments:
Post a Comment