
Wakati mamilioni ya watu duniani kote walikuwa
wakifuatilia na kuvutiwa na hotuba zilizokuwa zikitolewa katika shughuli ya
mazishi ya mzee Nelson Mandela, jumuiya ya kimataifa ya watu wenye ulemavu wa
kusikia imeelezea kughadhibishwa kwake na kile walichosema kuwa mkalimali wa
lugha ya alama aliyetumika katika shughuli hiyo alikuwa mkalimani bandia.
Kwa mujibu wa ripoti iliochapishwa kwenye mtandao wa SBS
News wa Australia, mlemavu kutoka Afrika Kusini na ambaye ni mwanachama wa Tawi
la Vijana la Shirikisho la viziwi duniani, Braam Jordaan, alisema kuwa
mkalimani huyo alikuwa akijitengenezea alama zake mwenyewe ambazo hazipo kabisa
kwenye lugha ya alama.
Jordaan anadai kuwa ishara za mikono, uso na harakati za
mwili hazikuwa zikifuata kile kilichokuwa kikisemwa na mzungumzaje, na kwamba
tukio hilo limetia aibu katika shughuli hiyo muhimu kwa taifa lake.
Mwakilizi wa Jumuiya ya Wakalimani wa Lugha ya Alama
ulimwenguni, Sheena Walters naye pia aliuambia mtandao wa SBS kuwa harakati za
mikono zilizokuwa zikitumiwa na mkalimani hazitambuliki katika aina yoyote ya
lugha ya alama.
Sheena alisema kuwa lugha nyingi za alama duniani zina
muundo na mfumo unaofanana na kwamba mkalimani huyo alikuwa akirudiarudia alama
zilizoonekana kutofahamika au kuonekana kwa wanaomfuatili.
Wakati shughuli za mazishi zikitangazwa moja kwa moja na
vyombo vingi vya habari ulimwenguni, wanachama wa jumuiya hiyo ya viziwi
walimiminika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuelezea hasira zao juu ya
tukio hilo.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, chama tawala
cha Afrika ya Kusini, ANC kimekuwa kikimtumia mkalimani huyo, na kiliwahi kulalamikiwa
juu ya udhaifu wake.
0 comments:
Post a Comment