Mwaka 2009 nikiwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya POAC
nilikuta utamaduni wa Mashirika ya Umma/Taasisi za Serikali kuwalipa wabunge
wanapoitwa kwenye kamati. Niliwashitaki Wabunge PCCB kwa matumizi mabaya ya
madaraka na kujilipa posho ambazo hawastahili maana Bunge linakuwa limelipa.
PCCB wakazuiwa uchunguzi wao na Spika Sitta, hata hivyo utamaduni huo ulikufa
na siku hizi hakuna kitu kinachoitwa 'Parliamentary Expenses' kwenye mahesabu
ya mashirika yote ya Umma.
PAC ilipiga marufuku Taasisi za Serikali au Mashirika ya
Umma kulipa wabunge kwa kazi za kibunge. Hivyo hakuna hata mjumbe mmoja wa PAC
anayelipwa posho na Taasisi yeyote ya Serikali kwa kazi za kibunge. Wajumbe wa
PAC wanalipwa posho kama kamati nyingine, na posho za vikao mimi sichukui maana
nimezikataa bungeni, nimezikataa Halmashauri ya Wilaya Kigoma, nimezikataa
Baraza la Ushauri la Mkoa wa Kigoma. Hata nikialikwa na NGOs kwa kazi zangu za
ubunge sichukui posho yeyote. It is a matter of principle!
Sipendi hata kidogo kulumbana na wabunge wenzangu kuhusu
suala hili. Ni jambo la hiari ya mtu kuchukua au kutochukua posho. Hebu
tujielekeze kutatua kero za wananchi badala ya kulumbana kunakosababisha
tutunge uongo ili tu kulilia posho. Mbunge anayelilia posho hastahili kuwa
mbunge. Akatafute kazi nyingine....
0 comments:
Post a Comment