Mkutano na waandishi wa habari: Mhe Zitto Kabwe na Dk
Kitila Mkumbo
Taarifa inatolewa kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe pamoja na
Dk Kitila Mkumbo watakutana na wahariri na waandishi wa habari kesho siku ya
Jumapili tarehe 24 Novemba 2013. Watatumia nafasi hii kutoa maoni na msimamo
wao kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ya hivi karibuni.
Mkutano huu na waandishi wa habari utafanyika katika
Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kuanzia saa5.00 asubuhi.
Imetolewa na ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe, Dar es Salaam.
Jumamosi, 23 Novemba 2013.
Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment