
Mtandao wa India today umechapisha habari kuwa Polisi
mjini Mumbai inawashikilia Watanzania wawili waliokamatwa na madawa ya kulevya
baada ya mwenzao wa tatu kufariki dunia.
Taarifa zinasema kuwa, baada ya polisi na kikosi maalumu
cha kudhibiti madawa ya kulevya kutonywa, waliwakamata katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Chatrapati Shivaji mjini Mumbai.
Miongoni mwa Watanzania hao, wawili walikuwa wamebeba
madawa ya kulevya na walikuwa wakisafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la
Ethiopia. Baada ya kuhojiwa kwa muda wa saa 5, bado hawakukiri kubeba madawa. Ndipo
walipopewa chakula na maji ili kujiridhisha.
Wabeba madawa huwa wanakataa kula au kunywa kwa sababu
ya kuhofia madawa kupasukia tumboni na kusababisha kifo. Mmoja kati yao
alikubali kula.
Baadaye watatu hao walipelekwa mahakamani, lakini yule
aliyekubali kula chakula aligoma na kujaribu kutoroka. Ghafla alianguka nje ya
mahakama na kufa katika hali iliyoonekana kuwa ni kuzidiwa na madawa. Inasemekana
marehemu alikuwa amebeba kete 20 mpaka 25 za madawa.
Hali ya mtu wa pili ilizidi kuwa mbaya na alipelekwa
hospitali ya JJ Jumatatu usiku. Baada ya vipimo vya X-ray na CT-scan, ilibainika
kuwa alikuwa amebeba kete 100 tumboni.
Mtu wa tatu ni mwanamke wa makamu. Inaelezwa kuwa
anahojiwa tofauti na wengine. Yeye hakubeba madawa, ila alikuwa pamoja nao, akiwasindikiza
hao wengine, ambao ni wanaume.
0 comments:
Post a Comment