
KWA uchache watu 24 wamepoteza maisha na wengine 28
kujeruhiwa baada ya treni ya mizigo kuligonga basi dogo pamoja na gari ndogo la
mizigo kusini mwa mji mkuu wa Misri, Cairo.
Kwa mujibu wa televisheni ya taifa pamoja na polisi,
treni hiyo ilikuwa ilikuwa ikitokea katika mji wa Bani Swaif na kuyagonga
magari katika wilaya ya Giza, kilometa 40 (maili 25) kutoka mji wa Cairo.
Majeruhi wengi ni ndugu wa familia moja waliokuwa
wakisafiri katika basi wakitokea harusini.
Treni hiyo ilikuwa imebeba vifaa vya ujenzi, na wizara
ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imesema kuwa inachunguza chanzo hasa cha ajali
hiyo.
Mkuu wa mamlaka ya usafiri wa reli nchini humo, Hussein
Zakariya, ameliambia shirika la habari la nchi hiyo, MENA, kuwa magari hayo
yalikuwa yakijaribu kuvuka eneo la reli ndipo yalipokutwa na zahma hiyo.
Usafiri wa reli nchini Misri unaelezwa kuwa na usalama
mdogo ambapo mwaka 2012 wizara ya uchukuzi ya nchi hiyo ilikosolewa vikali
baada watu 50, wengi wakiwa watoto, walipofariki dunia baada ya treni kuligonga
basi la shule mjini Cairo.
Ajali mbaya kabisa kutokea nchini humo iliua watu 360
mwaka 2002, baada ya mabehewa yaliyokuwa yamebeba abiria kuwaka moto.
0 comments:
Post a Comment