MLIPUKO wa volkano umeibua kisiwa kidogo jirani na pwani
ya Japan. Walinzi wa Pwani ya Japan wametoa tahadhari baada ya kisiwa hicho
kipya kutemea mvuke, moshi mweusi, majivu na mawe.
Kisiwa hicho kipya ni sehemu ya visiwa vingine
vinavyojulikana kama Visiwa vya Bonin katika eneo la Ogasawara. Bonin ni kundi
la visiwa 20 ambavyo havina wakazi na vipo kilometa 1,000 kutoka mji mkuu wa
Japan. Kisiwa hicho kipya kinakadiriwa kuwa na mita 200 kwa kipimo cha diameter.
Wataalamu wanasema kuwa huwenda kisiwa hicho kikatoweka
haraka au kikaendelea kuwepo na kuwa sehemu ya visiwa hivyo vingine.
![]() |
Moshi wa volkano kutoka chini ya bahari iliyotengeneza
kisiwa kipya kwenye pwani ya Nishinoshima, nchini Japan leo.
|
Tukio hilo lililotokea leo ni la kwanza katika eneo hilo
tangu miaka ya 1970. Harakati nyingi za volkano katika hilo huwa hayabainiki au
kuonekana kwa ababu mengi huishia ndani ya kina kirefu cha bahari.
Serikali ya Japan inaonekana kuwa makini sana na umiliki
wa maeneo kwa sababu tayari ina imekuwa katika migogoro kadhaa ya mipaka na
majirani zake. Hata hivyo, imelipokea tukio hilo na kulifurahia.
"Iwapo kitakuwa kisiwa kamili, tutafurahi kwa
sababu tutakuwa tumeongeza eneo la nchi yetu," alisema msemaji wa
serikali, Yoshihide Suga.

0 comments:
Post a Comment