![]() |
| Binti anayedai kubakwa na Prof. Kapuya |
Ndugu wanahabari,
Baada ya kumshukuru na kumtukuza mwenyezi Mungu mwingi
wa rehema. Natanguliza salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu mwanazuoni
na mwanaharakati mwenzangu Dkt Sengondo Mvungi aliyetangulia mbele ya Haki siku
chache zilizopita huko Afrika ya kusini.
Ndugu zangu wanahabari, Wengi mnanifahamu na kuifahamu
vema historia yangu katika utendaji kazi na utumishi wa umma wa Watanzania.
Nimekuwa nikiitumikia nchi yangu kwa kipindi kirefu katika Nyanja na sekta
mbali mbali kuanzia Darasani mpaka kwenye siasa. Kwa msingi huo, mimi Profesa
Juma Kapuya, siku zote ninajikuta mwenye wajibu endelevu wa kuendelea
kulitumikia Taifa langu kila siku mpaka kufikia mwisho wa Nguvu zangu.
Ndugu wanahabari, Hivi karibuni nikiwa huku jimboni
kuendelea na shuhuli za utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kumezuka
Tuhuma kadhaa zilizoelekezwa dhidi yamgu zikiasisiwa na wanasiasa wenzangu wa
ndani na nje ya chama changu ili kudhoofisha juhudi na utendaji wangu wa kila
siku. Tuhuma hizo zisizokuwa na kichwa wala miguu na pia kutokuwa na ukweli
wowote, wamekuwa wakizitoa kwa kumtumia msichana anayedai amefanyiwa vitendo
visivyofaa na mimi. Mimi simfahamu na sijui hizi shutuma zinatokea wapi.
Ndugu wanahabari,
Kwa tamko hili ninapenda kuwaambia kuwa nimefedheheshwa
sana na uwezo mdogo wa kisiasa unaofanywa na hawa watu kwa kuwa dhamira yao
haitatimia. Napenda niwakumbushe ndugu zangu kwamba tunaelekea kwenye uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015 na wapinzani wangu wameanza kunichafua ili nionekane sifai.
Ninapenda kuwaambia watanzania na wananchi wa jimbo langu kuwa wanatakiwa
wazipuuze taarifa hizi kwa kuwa hazina ukweli wowote na kwamba ni za kutungwa
zenye lengo la kunidharirisha na kuniondolea heshima yangu niliyojijengea
kwenye jamii kwa kipindi kirefu sasa. Waswahili wanasema dawa ya mjinga ni
kumpuuza
Na hili linajidhihirisha zaidi kwa habari hii kuandikwa
na chombo kimoja tu cha habari kinachotumiwa na chama kimoja cha siasa na
baadhi ya wanasiasa wa chama changu wasiokitakia heri chama chetu, naomba
kuwashukuru na kuwapongeza vyombo vingine vya habari kwa umakini wenu wa kuwa
na nauelewa wa kutoandika kitu bila kukifanyia uchunguzi na kubaini ukweli
ulivyo. Chombo hiki cha habari kiliwahi kuripoti mwaka jana kuwa kuna mitambo
imeingizwa nchini inayoweza kuandika ujumbe na kisha kuufanya uonekane umetoka
kwenye namba Fulani, kwa kipindi kile sikuwaelewa, lakini sasa ninawaelewa na
nimewaona kuwa wako sahihi na wao ndio waliouingiza mtambo huu na sasa wameamua
kuutumia dhidi yangu kwa kutengeneza meseji na kuzihusianisha na mimi.
Ninaamini ukweli utawaumbua muda si mrefu.
Ndugu wanahabari,
Nimeijenga heshima yangu na familia yangu kwa jamii
yangu kwa kipindi kirefu mno, kwa hivyo siwezi kuruhusu heshima niliyoijenga kwa
miongo kadhaa karibiwa na kupotezwa na watu wachache tena kwa muda mfupi namna
hii. Hivyop basi nimechukua hatua za kisheria kuhakikisha heshima yangu
inaendelea kulindwa na utu wangu unaheshimiwa. Nimemwagiza mwanasheria wangu
afungue kesi na tayari amewashitaki watu wote wanaohusika kwenye mpango huu na
tayari wameshapokea taarifa ya kuitwa mahakamani. Nitaendelea kuwachukulia
hatua kali za kisheria watu wote watakaoendelea kutaka kujipatia umaarufu ama
wa kisiasa au wowote ule kwa kutumia jina langu. Hayo yote ni kwa kuzingatia
ukweli kwamba nchi yetu inaendeshwa kwa misingi ya kisheria na kufuata na
kuheshimu haki na wajibu wakila mmoja wetu. Kwenye hilo ninawaambia ‘’janja yao
nimeigundua, na hawatafanikiwa’’ Ninatoa Rai kwa yeyote mwenye kuona hilo jambo
lina ukweli alipeleke kwenye vyombo husika ili lishuhulikiwe kwa mujibu wa
sheria na sio kutumia vyombo vya habari kuchafuana. Mwisho ninasisitiza kuwa
nitaendelea kuilinda na kuitetea heshima yangu niliyojijengea kwa jamii kwa
muda mrefu sasa na sitaruhusukuiona ikiharibiwa na wajanja wachache kwa maslahi
yao binafsi. Tuendelee kuijenga nchi
yetu, Mungu Ibariki Tanzania.
Imetolewa leo
tarehe 15.11.2013 nami
Prof. Juma A.Kapuya
Mbunge – urambo magharibi
S.L.P 45 Kaliua Tabora
Simu 0784993930


0 comments:
Post a Comment