![]() |
| Waethiopia wakiandamana mjini Addis Ababa kupinga mauaji ya wenzao waliouawa nchini Saudia Arabia |
POLISI nchini Ethiopia wametumia nguvu kutawanya mamia
ya wananchi wa nchi hiyo waliokuwa wakiandamana kupinga mashambulzi
yanayowalenga wafanya kazi wa Kiethiopia nchini Saudi Arabia.
Hayo yanakuja baada ya Waethiopia kukusanyika nje ya Balozi
wa Saudia mjini Addis Abba kupinga kamata kamata inayofanywa na utawala wa Riyadh
dhidi ya wahamiaji haramu.
Maandamano hayo yaliitishwa na Chama cha upinzani cha
Vuguvugu la Bluu baada ya Waethiopia watatu kuua nchini Saudi Arabia. Waandamanaji
walitoa wito wa kususia na kuzifunga biashara za Wasaudia nchini mwao. Wanaharakati
wanasema kuwa polisi walifanya haraka sana kuyasambaratisha maandamano hayo.
Kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa chama hicho, Getaneh
Balcha, zaidi ya waandamanaji mia moja, wakiwemo mwenyekiti wa chama hicho cha
upinzani na makamu wake wamekamatwa.
"Polisi walikuja na kutupiga, na sasa zaidi ya watu
100 wameshikiliwa katika kituo cha polisi,” alinukuliwa afisa huyo wakati
akiongea na vyombo vya habari.
Wiki iliyopita, serikali ya Ethiopia ilithibitisha kuwa
raia wake watatu waliuawa katika makabiliano na polisi wa Saudia.
Vifo vyao vilitokana na kamata kamata inayoendelea
kufanywa na utawala wa Riyadh dhidi ya wahamiaji haramu wapatao elfu 23 wa Ethiopia
pamoja na raia wengine wa kigeni. Waethiopia wengi husafiri kwenda Mashariki ya
kati kila mwaka kutafuta kazi.

0 comments:
Post a Comment