![]() |
| Fatima Maleh alifanyiwa vipimo na kupata cheti kilichoonesha kuwa ana homni za kiume. |
Na Kabuga Kanyegeri
MCHEZA soka wa kike nchini Tunisia, Fatima Maleh,
ametangaza kwenye radio moja ya kitaifa kuwa yeye ni mwanaume, ambaye
ameandikishwa rasmi katika taarifa za kiraia kama Mohammad Ali.
Maleh mwenye umri wa miaka 29 alipozaliwa aliandikishwa kama
mtoto wa kike, ambapo familia yake, marafiki zake na wanafunzi wenzanke
walimchukulia hivyo kwa miaka mingi.
“Nilipokuwa mtoto kila kitu kilikuwa sawa sawa, lakini
mambo yalianza kubadilika nilipofikia umri wa baleghe,” Maleh alikiambia kituo
cha habari za michezo, Radio Nationale.
“Nilipovuka umri wa miaka 12 na 13 hakuna kilichotokea,
nikaanza kujiuliza maswali, lakini sikupata majibu,” aliongeza kusema.
“Lakini nilianza kuhisi kuwa mimi sio mwanamke umri
wangu ulipoongezeka kidogo na kuanza kuhisi kuvutiwa na mabinti,” alisema
Maleh.
Alipokuwa sekondari, alianza kupenda kama watoto wa
kiume. Alipenda kukaa na wavulana na kucheza nao soka, anasema.
Katika mji wake wa nyumbani wa Tataouine, unaopatikana
kusini mwa Tunisia, haikuwa rahisi kwake kuandamana na wavulana. “Katika mji wa
Tataouine sikuweza kucheza na wavulana; walikuwa wakinipiga kila ninapokwenda
kucheza nao,” anasema.
Maleh alianza kuwa mchezaji wa kimataifa akichezea
katika klabu moja katika nchi moja ya Ghuba.
Aliwaficha wachezaji wa klabu yake ya wanawake na kwamba
hakuwa akijisikia raha anapokuwa katika
chumba cha kubadilishia nguo.
Baada ya miaka mingi ya usumbufu wa kisaikolojia kuhusu
suala la kutaka kubadilisha jinsia, hatimaye alianza mchangato wa kubadilisha
jinsia yake kwa taratibu za kiserikali kabla ya kuiweka hadharani siri yake.
Hatua ya kuingia katika mahusiano na mkewe mtarajiwa
ilimfanya azidi kuliweka hadharani suala hilo.
Mwaka 2008 alifanyiwa vipimo na kupata cheti
kinachomuonesha kuwa alikuwa na homoni nyingi za kiume na sifa za misuli ya
mwili wake kuwa ni ya kiume.
“Via vyangu vya uzazi vinaonekana zaidi kuwa kama vya
mwanaume,” alisema.
Kutokana na ceti hicho, Maleh aliweza kupata idhini ya
mahakama ya kubadilisha rikodi za jinsia yake katika kitambulisho chake za taifa
pamoja na nyaraka nyingine.
Anasema kuwa Juni
24, 2013 alifanikiwa kupokea kitambulisho chake kipya kikiwa na jina lake
alilochagua la Mohammad Ali.
CHANZO: Al-Arabiya

0 comments:
Post a Comment