
Naibu wa Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Libya ametekwa
nyara akiwa pamoja na mmoja wa viongozi waliooongoza mapinduzi dhidi ya Kanali
Muammar Gadafi nchini humo. Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa,
maafisa hao waandamizi wa Libya wametekwa nyara leo mjini Tripoli. Huku hayo
yakiripotiwa, habari kutoka Tripoli, mji mkuu wa Libya zinasema kuwa, hali ya
wasiwasi imerejea mjini humo baada ya kutulia kwa muda mfupi.
Kwa siku mbili mfululizo mji huo umeshuhudia mapigano
kati ya pande hasimu yaliyopelekea zaidi ya watu 40 kuuawa na karibu laki tano
wengine kujeruhiwa. Leo wananchi wa Libya wameendelea kuwazika watu waliouawa,
maziko ambayo yameambatana na maandamano ambapo wakazi wa mji huo wameitaka
serikali dhaifu ya nchi hiyo ikabiliane vilivyo na wanamgambo wenye silaha.
Wananchi hao wametishia kufanya uasi wa nchi nzima kama
serikali na makundi yenye silaha yatashindwa kufikia makubaliano ya kurejesha
amani katika nchi hiyo tajiri kwa mafuta ya kaskazini mwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment