![]() |
| Boeing 737 |
WATU wasiopungua 52 wamepoteza maisha baada ya ndege
aina ya Boeing 737 kuanguka nchini Urusi.
Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Majanga na masuala ya
dharura, Irina Rossius, ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Tatarstan
Airlines ilipata ajali hiyo katika mji wa Kazan, katikati mwa Urusi na kuua
watu wote waliokuwemo, ambao ni wafanyakazi 6 na abiria 46.
Mamlaka zinasema kuwa ndege hiyo ilijaribu kutua mara
mbili lakini ikashindwa na kuanguka katika jaribio la tatu.
Ndege hiyo iliyokuwa imetoka katika uwanja wa ndege wa
Domodedovo, ilishika moto baada ya kuanguka katika mji wa Kazan, karibu
kilometa 720 mashariki mwa mji mkuu wa Urusi, Moscow.
Hakujatolewa dalili zozote zinazoweza kuwa chanzo cha
ajali ya ndege hiyo.

0 comments:
Post a Comment