KIONGOZI mwandamizi wa kundi la wapiganaji wa mtandao wa
Haqqani, nchini Pakistan, wenye mafungamano na Talibani amepigwa risasi na
kuuawa.
Maafisa upelelezi wa Pakistan wanasema kuwa Nasiruddin
Haqqani, ndugu wa Sirajuddin Haqqani, ameuawa
jirani na mji wa Islamabad mwishoni mwa juma.
Duru zinasema kuwa mwili wake ulipelekwa katika mji wa Miranshah,
mji mkubwa katika jimbo la Kasikazini la Waziristan kwa ajili ya mazishi.
Mauaji ya kiongozi huyo yanakuja siku kadhaa baada ya shambulizi
la ndege za Marekani zisizokuwa na rubani (drone) kumuua kiongozi wa kundi la
Taliban nchini Pakistan, Hakimullah Mehsud, pamoja na watu wengine wanne katika
eneo la kaskazini magharibi mwa Pakistan lenye hali mbaya kiusalama.
Mtandao wa wapiganaji wa Haqqani, wenye mafungamano na
wapiganaji wa al-Qaeda, umekuwa ukifanya mashambulizi makali ndani ya Pakistan
na katika nchi jirani ya Afghanistan.

0 comments:
Post a Comment