
Kwa cuache watu 3 wamepoteza maisha na wengine kadhaa
kuejruhiwa baada ya kimbunga kupiga katika maeneo ya kati na kusini mwa jimbo
la Illinois nchini Marekani.
Kwa mujibu wa mkuu wa idara ya masuala ya dharura ya
jimbo hilo, Jonathon Monken, watu watatu walifariki dunia katika mji wa Washington
na kusema kuwa idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka na kuwaonya watu kuchukua
hatua mbalimbali za tahadhari.
Aidha, kimbunga hicho kimesababisha uharibifu mkubwa wa
majengo katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, na watu 37 wameripotiwa
kujeruhiwa vibaya sana.
Kimbunga hicho kilifuatia tahadhari mbalimbali
zilizokuwa zimetolewa na mamlaka za hali ya hewa na kuwataharidha wakazi kuwa
kimbunga hicho kilikuwa kikienda kwa mwendo wa kasi kubwa.
0 comments:
Post a Comment