Tunawashukuru watanzania kwa kufuatilia kinachoendelea
ndani ya CHADEMA. Nawapa pole wote waliokwazwa na jambo hili, na ninawashukuru
wote walionipa pole na kunitia moyo. Ninawashukuru pia walionilaumu na ni
vizuri kunyosheana vidole na kuwekana sawa pale ambapo moja wetu anaonekana
kukwamisha harakati za mabadiliko.
Haya ni mawimbi katika harakati za mabadiliko na
ninaamini yatapita na hayatayumbisha mchakato wa kusimika mfumo wa demokrasia
hapa nchini kwetu.
Ninashauri tuwe na subira katika kutoa hitimisho na
hukumu katika jambo hili. Mpaka sasa tumekwisha kupata upande mmoja juu ya
kilichotokea. Vuteni subira nasi tuseme ndipo mpitishe hukumu. Mungu akijalia
tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari wakati wowote kabla ya wiki ijayo na
tutaeleza upande wetu, na hasa kutoa maoni yetu juu ya kile kilichotamkwa jana
kwamba sisi ni wahaini na wahujumu ndani ya chama chetu.
Kwa sasa tambueni tu kuwa mie binafsi bado nipo imara
katika kuhakikisha kwamba siwi kikwazo na ninachangia kikamilifu nguvu zangu
katika harakati takatifu za mabadiliko hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment