Zaidi ya watoto 60 wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika
handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni ,Dar es
Salaam, ambalo ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba.
Utekaji huo unadaiwa kufanywa na raia wa kigeni
(Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao hufungiwa katika
vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa.
Mtoto Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano
Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam na mdogo wake
Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo, ndio waliofichua
ukatili huo mwishoni mwa wiki.
Watoto hao walitekwa na Wazungu w
awiliasubuhiyaSeptemba2mwaka huu, wak ati wakiendas huleni n akufan ikiwa
kutoroka katikaj engohiloSeptemba 23 mwaka huu.
Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo
kidogo cha Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani
ya jengo hilo kuna watoto wengi wa kike na kiume.
Walisem a w atoto hao wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa
kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia
wazazi wao ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa.
"Jumba hili limejengwa ndani ya handaki, tulikuwa
tukifanyishwa kazi ngumu na nzito, usiku tunajaza maji katika mapipa mengi na
kubebeshwa ndoo kupanda na kushuka kilima.
"Tunapigwa fimbo, wasichana wanafungiwa kwenye
vyumba, wanabakwa na kulawitiwa kwa zamu na Wazungu, tunachomwa moto (alionesha
mguu wake uliochomwa) na kupigwa shoti ya umeme tunapowaulizia wazazi
wetu," alisema Emmanuel kwa uchungu akitokwa na machozi.
Aliongeza kuwa, asubuhi ya Novemba 23 mwaka huu, katika
jengo hilo kulitokea kutokuelewana kati ya Wazungu na Waswahili ambapo mswahili
mmoja aliwatisha wazungu kwa kuwaambia polisi wanakuja hivyo walikimbia na
kuacha mlango wazi.
"Hali hiyo iliniwezesha mimi, mdogo wangu na watoto
wengine wachache waliokuwa na nguvu kufanikiwa kutoroka, nilimshika mkono mdogo
wangu ambaye alionekana kuchoka nikamvuta.
"Watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu nao
wakatoka, wengi hawakuweza kutoka kutokana na kukosa nguvu, wanaumwa, wana
vidonda vikubwa mwilini kutokana na kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme,
wasichana hawakuweza kabisa kutoka kwa kuwa wamefungiwa ndani ya vyumba,"
alisema Emmanuel
Aliongeza kuwa , alijikokota taratibu na mdogo wake
mbali ya maumivu makali waliyonayo akatokea Mswahili mmoja ambaye alikuwa na
gari lenye vioo vyeusi akawaambia wapande ili awatoroshe.
"Tulipanda gari hilo akatushusha darajani mpakani
mwa Manispaa ya Kinondoni na Wilaya ya Kibaha, jirani na mzani eneo ambalo sisi
hatukuwa tukilifahamu...dereva huyo alituambia gari limeishiwa mafuta hivyo
alitutaka tumsubiri aende kuyanunua.
"Tulitembea kidogo tukiwa hatujui tunakokwenda...
tulikaa kando ya barabara kutokana na uchovu pamoja na njaa kali kwani katika
jengo hilo mbali na kazi nzito tulizokuwa tukizifanya na mateso mengi, mlo
ulikuwa mmoja tu kwa siku.
"Tulikula saa 10 jioni, wali na maharage...tukiwa
kando ya barabara, nilisikia sauti ya baba yangu wa kufikia, dereva wa magari
makubwa yanayobeba kokoto ikiniita.
"Nilidhani naota kumbe ilikuwa kweli, alikuja
akatukumbatia akalia kwa uchungu kwa namna tulivyokuwa tumechoka na afya
kuzorota, akatupeleka polisi ambapo tulipatiwa maji tukaoga na kupewa chakula
kizuri na kitamu, tukala na kupata nguvu za kuzungumza vizuri," alisema
Emmanuel.
Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa
yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa
ndani ya jumba hilo la mateso.
Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili
kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.
Mama mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye
anafanya shughuli za mama lishe, njia panda y a Ba r a k u d a , Ta b a t a
Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto
hao bila mafanikio.
"Nimepoteza fedha nyingi kwa kuwatafuta na
kutapeliwa mara kadhaa katika kuhangaika," alisema Godianus huku akitokwa
na machozi ya furaha katika Kituo kidogo cha Polisi Maili Moja.
Alisema zaidi ya watoto saba walipotea katika mtaa wao,
wawili wakapatikana baada ya wiki mbili, wengine wakiwemo wanaye wakawa
hawajapatikana na kuomba Serikali ilichukulie kwa uzito suala hilo ili kubaini
kundi linalowateka watoto na kuwatesa.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri
kutokea kwa tukio hilo na kuanza kulifanyia kazi kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.
Alisema makachero wa polisi wamewahoji watoto hao ili
kupata maelekezo ya kufika katika andaki hilo na kuwataka watu wote wenye
taarifa za eneo hilo watoe ushirikiano.
JAMII FORUMS/ GAZETI LA MAJIRA

0 comments:
Post a Comment