Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo
kutakuwa na visingio vingi, ukweli ni kwamba "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO
INATAWALA AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili
kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa
kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara
kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo
haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua
hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo
akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili
ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. Kwenye
chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Pale bungeni
watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu waziri kivuli
hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu. Lakini walioishia
kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya
chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na
matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa. Vijana wahitimu wa
vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote wa
hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa.
Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu,
Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni
rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio
utakwepo kwenye list. I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and
consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi
kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga
watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko mchango
wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko mafunzoni. Sio adhabu
nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi. Haya ndio
madhara ya AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA, HOFU NDIO HUTAWALA
mwigulu wewe pia akili yako si kubwa kama unavo fikiri....nakuona mdogo sana katika kupambanua mambo, zaidi sana umekuwa mropokaji>>>>>kila la kheri katika uropokaji wako ila nakupa angalizo kwamba 2015 huna jimbo wewe
ReplyDelete