
WATU kumi wamethibitika kupoteza maisha kufuatia ajali
iliyoihusisha treni na daladala katika eneo la Umoja mjini Nairobi, Kenya.
Mkuu wa kikosi cha reli, Kirimi Ringera amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa, miongoni mwa waliopoteza maisha ni
wanaume watano na wanawake watano, huku wengine 21 wakiwa wamejeruhiwa vibaya
sana na kupelekwa hospitalini.
Ajali hiyo ilitokea wakati daladala ikijaribu kuvuka reli
ndipo treni ilipoigonga.
Kwa mujuibu wa mashuhuda, daladala hiyo ilisukumwa
umbali wa mita 500 kutoka kwenye eneo la ajali.
CHANZO: KTN Kenya
0 comments:
Post a Comment