Tanzania imetoa msimamo juu ya jumuiya ya afrika
mashariki na kusisitiza haitatambua maamuzi yoyote yatakayojadiliwa na
kuamuliwa na baadhi ya nchi wanachama nje ya utaratibu wa jumuiya.
Akijibu swali la mbunge wa Viti maalum mhe. RUKIA
AHMED nini msimamo wa serikali juu ya
mambo yanayohusu jumuiya ya Afrika Mashariki kujadiliwa nakutolewa uamuzi bila
ya Tanzania kushiriki.
Waziri wa Afrika Mashariki Mheshimiwa SAMWEL SITTA
Amewataka wabunge na watanzania kutambua Tanzania iko makini katika kufuatilia
yanayojitokea katika ndani ya nchi wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki.
Akijibu swali la Mmbunge wa Same mashariki mhe anne
kilango malecela aliyehoji kwa nini Tanzania imekaa kimya katika kuhukua
maamuzi, mheshimiwa SITTA amesema serikali haijakaa kimya kuna hatua
inazichukua na kusisitiza mamlaka kuu wamekumaliana kutokushiriki katika vikao
vyote ambavyo nchi nyingine tayari wanaagenda zao.
Chanzo: ITV
0 comments:
Post a Comment