
Maghala mawili ya kuhifadhia nyuzi yaliyopo katika
kiwanda cha nyuzi mjini Tabora kinachomilikiwa na mwekezaji mwenya asili ya
kiasia, yameteketea kwa moto tangu saa 7 mchana na kusababisha hasara kubwa
ambayo haikujulikana mara moja.
Mkuu wa kikosi cha zimamoto manispaa ya Tabora Bw.
Farijara amesema kuwa katika harakati za kuzima moto huo usisababishe madhara
sehemu ya uzalishaji, moto huo haukuleta madhara kwa binadamu na chanzo bado
hakijajulikana.
Mmiliki wa kiwanda hicho amesema kuwa hasara
iliyojitokeza katika sehemu hiyo ni kubwa, lakini haitaathiri sehemu ya
uzalishaji kutokana kuwa na malighafi sehemu nyingineambazo hazijateketea kwani
sehemu iliyoteketea ni sehemu ya mali ambayo ilikuwa imesindikwa tayari.
Hata hivyo watumishi wa kiwanda hicho wamemshukuru Mungu
kutokana na moto huo kuwaka wao wakiwa mapumziko ya chakula, kwani ingeweza
kuleta madhara kwa maisha ya watu ambao hufanya kazi ndani ya maghala
hayo, huku wakisikitikia hasara
iliyojitokeza kwani ni sehemu ya uzalishaji wa kiwandani hapo.


CHANZO: ITV
0 comments:
Post a Comment