
JARIDA maarufu la Forbes la nchini Marekani limemchagua
Rais wa Urusi, Vladimir Putin kuwa mtu mwenye ushawishi zaidi duniani akimtangulia rais mwenzake wa Marekani, Barack Obama.
Leo Jumatano, jarida hilo limechapisha orodha ya watu 72
wakiwemo marais na viongozi wa mashirika na taasisi za kimataifa linalowaona
kuwa watu wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani kwa mwaka 2013.
Katika orodha hiyo, Putin ameshika nafasi ya kwanza
akifuatiwa na Obama katika nafasi ya pili na rais wa chin Xi Jinping ameshika
nafasi ya tatu.
Aidha, katika orodha hiyo, Papa Francis ameshika nafasi
ya nne, akifuatiwa na Kansela wa Ujerumani, Angela Markel, katika nafasi ya
tano.
0 comments:
Post a Comment