Na Rajab Ganga
Ni hatari kubwa kutumia kubeba madawa ya kulevya kwa
njia ya tumbo njia hii imewaathiri wengi ambao matokeo yake ni:
KIFO
Kifo hutokea kwa mbebaji wa madawa kwa njia ya utumbo
ambae humeza madawa haya ili kujizuzia na kukamtwa na vikosi vya usalama
wakitumia njia hiyo kuwa ni salama matokeo yake ni uzito kumzidi mbebaji na
baadhi ya tembe kuingia katika njia ya nje ya utumbo ikipelekea kupasuka kwa
tembe hizo wanasema kurishai.
MATATIZO YA TUMBO
mbebaji wa madawa tumbo lake mara kwa mara huhisi
maumivu kutokana na ugumu wa tembe hizo zinapozama tumboni kwa muda mrefu na
kipindi kirefu, tembe hizo husongamana na kuta za utumbo na kusababisha
maumivu.
KULEGEA KWA NJIA YA HAJA KUBWA
Kitendo cha kutoa madawa kwa njia ya haja kubwa
hupelekea mbebaji kulegea sehemu zake za haja kubwa na matokeo yake mfumo wa
usafishaji wa haja kubwa hudhoofika na kusababisha maradhi ya fangasi, Cancer
na ugonjwa wa kushuka nyama ya haja kubwa maarufu Puru, hayo ni baadhi ya
matatizo makubwa yatokanayo na ubebaji wa tembe za madawa ya kulevya kwa njia
ya utumbo.
Hizi ni picha za kijana aliefariki akiwa ndani ya ndege
akiwa na madawa tumboni na kufanyiwa upasuaji.




0 comments:
Post a Comment