Na Rajabu Ganga
UONGOZI wa klabu ya soka ya African Sports ya jijini
Tanga umeomba wadau wa mchezo huo kujitokeza katika Kuidhamini klabu hiyo
ambayo inakabiliwa na hali ngumu kiuchumi na kupelekea kushindwa kukata kiu ya
mashabiki ya kufikia malengo ya kushiriki ligi kuu Tanzania bara.
Msemaji wa klabu hiyo kongwe Said Karisandasi akizungumza
kilabuni hapo barabara ya 12 jijini Tanga alisema kuwa klabu hiyo kwa sasa
inakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha za kuwezesha shughuli mbali mbali kilabuni
hapo.
Karisandas alisema timu
hiyo ambayo kwa sasa inashiriki ligi ya ngazi ya mkoa ikiwania ubingwa
huo utakaoiwezesha kushiriki ligi daraja la kwanza msimu ujao imekuwa na tatizo
la fedha katika kukidhi mahitaji ya kambi ya wachezaji pamoja na vifaa vya
mazoezi.
Aidha Karisandas alisema klabu hiyo inakaribisha
makampuni, mashirika mbali mbali pamoja na mdau mmoja mmoja kujitolea kudhamini
fedha taslimu na vifaa vya michezo.
Msimu uliopita klabu ya African Sports ilifanikiwa
kuibuka na ubingwa wa mkoa wa Tanga baada ya kutembeza kichapo kikali kwa timu pinzani na hatimaye
kumaliza ligi hiyo ikiweka kibindoni
alama 54 za ushindi ikifuatiwa na klabu ya Small Prison ya Maweni Tanga.
African Sports, maarufu kama Wana kimanumanu, ambao 1988-1989 ilifanikiwa kuchukua ubingwa
wa kombe la jamhuri Tanzania ipo mbioni kuhakikisha inarudi katika ushiriki wa
ligi kuu Tanzania bara baada ya kupoteza nafasi hiyo msimu wa mwaka 1991-1992.
0 comments:
Post a Comment