RAIS Robert Mugabe amesema kuwa serikali inatakiwa
kuweka adhabu kali zaidi kwa wabakaji na kupendekeza kuwa waleo wanaowabaka
watoto wahasiwe, akieleza kuwa hatua kali inatakiwa kuchukuliwa kukabiliana na
tatizo hilo linaloshamili.
Akizungumza baada ya ufunguzi rasimi wa Bunge siku ya
Jumanne, Mugabe alielezea kusitishwa kwake na ongezeko la matukio ya watu
wazima kuwanajisi watoto na kusema kuwa hatua hiyo itasaidia kukabiliana na
matukio hayo.
“Tutawawekea adhabu kali sana, hatukubali kabisa watoto
na wanawake kunajisiwa” alisema.
Mugabe alisema kuwa ni wakati wa kufikiria kuweka adhabu
kali zaidi akiongeza kuwa alikuwa tayari kuweka adhabu ya kuwahasi wabakaji.

0 comments:
Post a Comment