
Utafiti wenye kushangaza umebaini kuwa Uingereza ina zaidi ya mitandao nusu milioni ya ngono, na hivyo kuifanya kuwa nchi ya tatu dunia kwa huduma za ngono mtandaoni.
Jina la kikoa cha kitaifa (yaani domain) linaloishia na co.uk hutumiwa na zaidi ya kurasa (pages) milioni 52, zenye maudhui ya ngono, na hivyo kuifanya Uingereza kuwa miongoni mwa vituo maarufu sana dunia kuwa na tovuti za mambo ya kikubwa.
Kampuni inayosajili mitandao hiyo ya ngono inaitwa “Nominet UK” na ripoti hiyo inasema kuwa hakuna mipaka ya kusajili tovuti kwenye kikoa (domain) cha jina hilo la Uingereza.
Ni hivi karibuni tu serikali ya Uingereza ilizindua kampeni ya kitaifa ya kuzidhibiti tovuti zenye ngono na matusi kwa watoto.
Mshauri wa serikali kuhusu usalama wa intaneti kwa watoto, John Carr, amekuwa akiitolea wito Nominet kuzibana tovuti zenye maneno kama “kubaka” na kadhalika.
Ameitaka kampuni hiyo kukomesha janga la “uhuru kwa wote na kwa kila kitu.”
Waziri wa mawasiliano, Ed Vaizey aliitaka Nominet kueleza mipango yake kwa uwazi ili kuzuia hiyo “tabia chafu”.
Hili linatokea katika wakati ambapo Marekani ina takriban theluthi mbili ya tovuti zote za ngono ulimwenguni.
Hata hivyo, Uingereza ina mara sita ya mitandao ya ngono ikilinganishwa na Ujerumani, ambayo ni nne, na mara kumi ya Ufaransa ambayo ni ya tano.
0 comments:
Post a Comment