JE, MURSI ANAADALIWA KWENDA UHAMISHONI?



Gazeti la TIMES la Uingereza limeeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa Saudi Arabia ikampa hifadhi Dokta Muhammad Mursi katika kujaribu kutatua mgogoro unaoiandama nchi hiyo.

Katika makala iliyoandikwa katika mtandao wa shirika la habari la BBC, gazeti hilo limeongeza kusema kuwa japokuwa Saudia wanakichukia sana chama cha Udugu wa Kiislamu (Muslim Brotherhood), ila wanataka kutanzua mzozo unaoikabili Misri, kumuachia huru Mursi na kumuondolea mashitaka yanayomkabili, jambo linaloelezwa kuwa litatoa fursa kwa jeshi na serikali ya mpito kujadiliana na wafuasi wa chama hicho.

Saudi Arabia inasifika sana kwa kuwapokea viongozi mbalimbali waliofukuzwa katika nchi zao, isipokuwa wanapokuwa huko hawaruhusiwi kujihusisha na shughuli za kisiasa, na ni nadra sana viongozi hao kuonekana. Na hilo ndilo linalotamaniwa na viongozi wa jeshi la Misri ambalo halina nia ya kumruhusu Mursi kuwa na nguvu ya kisiasa kwa mara nyingine.


Aidha, kwa mujibu wa gazeti hilo, wale waliokutana na Mursi baada ya kung’olewa madarakani, wanasema kuwa bado ana imani kwamba atarejea tena madarakani, na kwamba huwenda akakubali kwenda uhamishoni kwa muda, ima nchini Uturuki au Qatar. Isipokuwa hakuna dalili za kwamba Qatar iko tayari kuingilia kati suala hilo au kumpa hifadhi ya kutosha.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment