JAPAN YAADHIMISHA MIAKA 68 YA MAANGAMIZI YA HIROSHIMA NA NAGASAKI






Japan inatarajia kuadhimisha miaka 68 ya mashambulizi ya bomu la atomiki yaliyofanywa na Marekani dhidi ya mji wa Hiroshima, tukio la kwanza kabisa la matumizi ya bomu hilo dhidi ya binadamu, lililosababisha vifo vya maelfu ya watu.


Maelfu ya watu, wakiwemo manusura, ndugu wa waathirika na maafisa wa serikali wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho hayo ya kila mwaka kwenye eneo la Kumbukumbu ya Amani ya Hiroshima, linalojulikana kama Kuba la Bomu la Atomiki leo Jumanne.


Mji wa Hiroshima uliteketezwa mnamo Agosti 6, 1945, baada ya bomu la atomiki kutupwa na Marekani kwenye mji huo na kuua watu wapatao 140,000 papo hapo na wengine kufariki baadaye kutokana na mionzi na saratani vilivyowaua taratibu. Siku tatu baadaye, bomu lingine la atomiki lilidondoshwa kwenye mji wa Nagasaki na kuua zaidi ya watu 70,000. 

Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika katika wakati ambao hisia kali dhidi ya nyuklia bado zinafukuta miongoni mwa raia wa nchi hiyo.


Tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha mawimbi ya tsunami lilipiga katika maeneo ya pwani ya kaskazini mwa Japan mwezi Machi 2011 na kusababisha janga la nyuklia kwa kuharibu  mifumo ya upoozaji katika kinu cha nyuklia cha Fukushima, na hivyo kusababisha uvujaji wa mionzi.




Mawimbi ya tsunami, yaliyopiga kwenye kinu cha nyukilia cha Fukushima Daiichi dakika 45 baada ya tetemeko la ardhi, yalizima jenereta za dharura kwenye kinu hicho.

Watu wapatao 19,000 walipoteza maisha au kupotea wakati wa janga hilo.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment