Mawasiliano baina ya viongozi wawili katika mtandao wa al-Qaeda yalisababisha kufungwa kwa balozi za Marekani katika nchi nyingi duniani. Mtandao wa habari wa aljaras.com umenukuu kile kilichoelezwa kuwa ni ripoti ya Marekani baada ya nchi hiyo kunasa mazungumzo ya simu kati ya kiongozi wa mtandao wa al-Qaeda, Ayman al-Dhawaahiri na kiongozi wa tawi la mtandao huo nchini Yemen, Naasir al-Wahshy. Inaelezwa kuwa katika mazungumzo hayo, al-Dhawaahiri alimtaka al-Wahshy kutekeleza mashambulizi ya aina yake dhidi ya maslahi ya Marekani na nchini za Magharibi ambayo yatakuwa makubwa zaidi kuliko yale ya Septemba 9.
Kwa hivyo, Marekani ilikuwa imepanga kuzifunga balozi zake katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika (kama vile Abu Dhabi, Oman, Cairo, Riyadh, Tehran, Doha, Dubai, Kuwait, Manama, Masqat, Sanaa na Tripoli) mpaka Jumamosi ijayo, kwa hofu ya mashambulizi ya a-Qaeda ambayo yangefanywa mwishoni mwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Aidha, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitoa taarifa ikitoa tahadhari ya kusafiri mpaka mwisho wa mwezi wa Agosti. Tokea Jumapili, imezifunga balozi zake katika nchi zipatazo 20.
Nchi kadhaa za Magharibi, kama vile Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, nazo pia zimefunga balozi zake mpaka mwisho wa wiki.
0 comments:
Post a Comment