35 WAUAWA KATIKA MAPIGANO NCHINI NIGERIA


Nigerian troops patrol the streets of the town of Baga in the northeastern Nigerian state of Borno. (File photo)
Askari wa Nigeria wakifanya doria katika mitaa ya mji wa Baga katika jimbo kaskazini mashariki la Borno.




Jeshi la Nigeria limesema kuwa kwa uchache watu 35 wameuawa katika mapambano kati ya jeshi hilo na wanamgambo kaskazini mwa nchi hiyo.


Jeshi hilo linasema katika taarifa yake leo Jumatatu kuwa katika mapambano hayo yaliyozuka katika maji wa kaskazini mashariki wa Bama baada ya kituo cha polisi kushambuliwa, polisi mmoja na wanamgambo 17 waliuawa.


Taarifa hiyo iliongeza kusema kuwa askari wawili na wanamgambo 15 pia waliuawa katika mapigano katika mji wa Malam Fatori kufuatia askari kushambuliwa. 

Miji yote miwili ipo katika jimbo la Borno nchini Nigeria, ambalo ni ngome ya kundi la wapiganaji wa Boko Haram. 


Jeshi linasema kuwa wakati wa mashambulizi hayo, wanamgambo walikuwa wamejihami kwa "silaha nzito" na vifaa mbalimbali vya milipuko.


Kwa zaidi ya miaka minne sasa, machafuko katika taifa hilo lenye wakazi wengi zaidi Afrika yamegharimu maisha ya watu wapatao 3,600, yakiwemo mauaji yaliyofanywa na vikosi vya usalama. 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment