WAZIRI AFUNGWA MIAKA 9 JELA KWA UFISADI



Ottoviano Del Turco, former Italian finance minister and governor of Abruzzo
Ottoviano Del Turco, aliyewahi kuwa waziri wa fedha wa Italia na gavana wa mkoa wa Abruzzo



Aliyewahi kuwa waziri wa fedha wa Italia, Ottoviano Del Turco, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa na nusu jela kwa kuhusika na vitendo vya hongo na rushwa katika sekta ya afya.



Ottoviano Del Turco alihukumiwa na mahakama moja katika mji wa Pescara jana Jumatatu kuhusiana na wizi wa kiasi cha yuro milioni 15 (dola milioni 19) katika mfumo wa fedha za sekta ya afya nchini humo.


Mbali na adhabu ya kifungo, ameamriwa kutoa zaidi ya kiasi cha yuro milioni 3 kwa hasara iliyotokea na amepigwa marafuku kutoshika wadhifa wowote wa umma kwa kipindi chote cha maisha yake.


Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Del Turco amekuwa katika kizuizi cha nyumbani baada ya mfanyabiashara mmoja kuwaambia waendesha mashitaka kuwa alikuwa amemhonga Del Turco kiasi cha zaidi ya yuro milioni sita (dola milioni 8). 

Kufichuka kwa habari hizo kulimlazimisha ajiuzulu ugavana wa mkoa wa Abruzzo baada ya kutawala kwa kipindi cha miaka mitatu. 

Vilevile, mahakama iliwahukumu washitakiwa wengine 8 wanaohusika na kesi hiyo, akiwemo  Vincenzo Maria Angelini, mtu aliyekiri kumhonga Del Turco. Alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu na nusu jela. 

Kabla ya kuwa gavana, Del Turco alikuwa mbunge wa Bunge la Ulaya mwaka 2004.


Vilevile alishika wadhifa wa waziri wa fedha kuanzia mwaka 2000 mpaka 2001 katika baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Giuliano Amoto. 

Italia imekuwa ikikumbwa na kashfa kadhaa za ufisadi zikiwahusisha maafisa na watumishi wa sekta ya umma. 

Miongoni mwa maafisa hao ni waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo kutoka mrengo wa kihafidhina, Silvio Berlusconi, ambaye mara kadhaa amekuwa akishitakiwa kwa makosa mbalimbali ya uhalifu.

 

Berlusconi ana hatari ya kukutwa na hatia baadaye mwezi huu, pindi mahakama ya rufaa itakaposikiliza mashitaka ya ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka yaliyowasilishwa dhidi yake.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment