UTAFITI: UCHAFUZI WA HEWA UNAVYOHATARISHA MAPAFU NA MOYO WAKO

 


Watafiti wa Ulaya wameonya kwamba uchafuzi wa hewa, hususan moshi unaotoka kwenye magari, huongeza hatari kubwa ya kusababisha saratani ya mapafu na maradhi ya moyo.

Timu ya kimataifa ya utafiti ilifanya uchunguzi 35 pamoja na taarifa za maelfu ya wagonjwa katika nchi 12, zikiwemo nchi za Ulaya, Marekani na China.

Uchunguzi huo uliofanywa kwa watu 300,000 kwa kipindi cha miaka 13 unaonesha kuwa maeneo ambayo kuna ongezeko la msongamano wa magari, wakazi wa maeneo hayo walikuwa na hatari kubwa ya kupatwa na saratani ya mapafu na moyo kushindwa kufanya kazi, kwa mujibu wa utafiti huo uliochapishwa katika jarida la kimataifa la masuala ya tiba la the Lancet.

Kiasi cha watu 2095 kutoka katika jumla ya watu walioshiriki walikutwa na tatizo la saratani ya mapafu.

Kwa wagonjwa waliohusishwa na matatizo ya moyo, uchafuzi wa hewa huifanya mishipa ya moyo kuwa dhaifu na kutofanya vizuri kazi yake ya kusukuma damu kuuzunguka mwili. Hali hii huelezwa kuwa ni matokeo ya shambulizi la moyo.

Hatari hiyo ni tishio kubwa zaidi kwa wale walio katika viwango vikubwa vya uchafuzi wa hewa ambapo gesi mbalimbali kama kaboni monoksidi, sulfuri  dioksidi, na gesi nyingine chafu zinaweza kuingia katika mapafu na kisha kwenda katika mfumo wa damu.


Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, uchafuzi wa hewa katika miji midogo na mikubwa huua watu milioni 1.3 kila mwaka duniani kote.


Wakati watu wapatao 30,000 nchini Uingereza hufariki dunia mapema kila mwaka kutokana na uchafuzi wa hewa, kiwango kibovu cha hewa kinaelezwa kuwa miongoni mwa sababu 10 za juu zinazosababisha vifo.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment