![]() |
| wafanyakazi wa afya wakiwa wamefunika pua na midomo yao wakiondoka katika kitengo cha dharura cha Hospitali ya Mfalme Fahad katika mji wa Hofuf, Kilometa 370 Mashariki mwa mji Mkuu wa nchi hiyo, Riyadh, Juni 16, 2013. |
Maafisa wa afya nchini Saudi Arabia wametoa tahadhari wakiwataka mahujaji kuvaa vitu vya kuziba pua na mdomo katika maeneo yenye msongamano wa watu ili kuzuia usambaaji wa virusi vikali vilivyoikumba nchi hiyo.
Wizara ya Afya ilitoa orodha ya mambo yanayotakiwa kufanywa na mahujaji wanaopanga kwenye kufanya ibada ya hijja katika juhudi za kuzuia kuenea kwa virusi aina ya Middle East Respiratory Syndrome coronavirus (MERS-CoV), vyombo mbalimbali vimeripoti.
Watu wenye umri mkubwa au wale wenye magonjwa sugu nao pia wameshauriwa kuakhirisha safari zao za hijja.
Mpaka sasa watu wapatao 38 wameshapoteza maisha kutokana na maambukizi hayo nchini Saudi Arabia.
Adiha, maafisa hao waliwataka watu kuchunga kanuni za afya, usafi, kutumia vitambaa wakati wa kupiga chafya na kukohoa, na kupata chanjo ya dharura.
Waumini wa dini ya Kiislamu hufanya ziara kwenye miji mitukufu ya Makka na Madina katika kipindi chote cha mwaka, lakini msimu mkubwa hasa utakuwa mwezi Oktoba mwaka huu, ambapo mamilioni ya Waislamu duniani kote wanatarajiwa kumiminika nchini humo kwa ajili ya ibada hiyo ya kila mwaka.
Kwa mara ya kwanza virusi hivyo viliibuka katika eneo la Mashariki ya Kati, na viligunduliwa mwezi Septemba mwaka 2012 kutoka kwa raia mmoja wa Qatar aliyekuwa amesafiri nchini Saudi Arabia.
Matukio kadhaa ya virusi hivyo yameripotiwa katika nchi za Saudi Arabia, Jordan, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Tunisia na Uingereza.
MERS-CoV ni virusi ndugu na virusi vya SARS. Matabibu wanafanya juhudi kubaini jinsi watu wanavyoambikizana virusi hivyo katika harakati za kutafuta tiba yake.
MERS-CoV ni virusi ndugu na virusi vya SARS. Matabibu wanafanya juhudi kubaini jinsi watu wanavyoambikizana virusi hivyo katika harakati za kutafuta tiba yake.
Virusi hivyo havionekani kuambukiza kama virusi vya SARS, ambavyo viliua kiasi cha watu 800 mwaka 2003.

0 comments:
Post a Comment