Klabu ya Manchester United leo imeweka mezani dau la yuro milioni 26 katika harakati za kumnyakua Cesc Fabregas.
David Moyes anataka kuimarisha utawala wake Old Trafford kwa kuhakikisha mchezaji huyo nyota wa Barcelona anakuwa windo lake la kubwa la kwanza.
Meneja mpya wa United ametangaza hatua yake hiyo baada ya kuwasili nchini Australia katika ziara ya kimichezo inayofanywa na klabu yake kabla ya kipenga cha msimu mpya wa Ligi Kuu hakijapulizwa.
Fabregas aliondoka Ligi Kuu ya Uingereza mwaka 2011 akitokea Arsenal kurejea kwao Catalonia.
Lakini ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Nou Camp na amekuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kuondoka katika kipindi hiki cha majira ya joto.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 26, msimu uliopita alikiri kuwa anaweza kuondoka Catalania kama wataweka wazi msimamo wao wa kutomhitaji tena.
Dau hilo la United linaweza kuongeza vita na Arsenal, ambao mwanzo walionekana kutaka kumrudisha kundini.

0 comments:
Post a Comment