MBINU YA AJABU YA KUWAKABILI WEZI WA WAKE NA WAUME ZA WATU

Hebu jaribu kuvuta picha hali anayokuwa nayo mume anapohisi kuwa kuna mwanaume anamfuatilia mke wake. Bila shaka unajua atakachokifanya. Lakini kama bado una mawazo ya mbinu ambazo wanaume wanaweza kuzitumia kujibu mapigo, huwenda mbinu hii itakushangaza sana.

Badala ya kutumia mabavu kumkabili mwizi wa mkewe, mwanaume mmoja katika jimbo la Illinois nchini Marekani alijibu mapigo kwa kutumia kichupa cha rangi.

Mwanaume huyo aliyeonekana kuwa mwenye hasira aliamua kwenda kwenye karakana (gereji) ya mwanaume aliyehisi kuwa anamfuatilia mkewe na kuandika ujumbe ufuatao kwenye mlango wa karakana hiyo.

'Don't e-mail my wife (Acha kuwasiliana na mke wangu)!!!!' mwanaume huyo mwenye hasira aliandika kwenye lango kuu la karakana hiyo.

Message received: A Reddit user shared a photo of a house in Illinois with garage doors tagged with a message for a man who apparently has been making advances to his wife, which read: 'don't e-mail my wife!!!!' and 'stop now'
Ujumbe umefika


Kwa lango dogo la upande wa kushoto aliweka maneno mengine kuonesha msisitizo, 'stop now (Acha sasa).'

Sasa jaribu kuvuta picha upande wa pili. Unadhani mke wa jamaa huyo atakapopoona ujumbe huo alioandikiwa mumewe atachukua hatua gani?

Inaonekana kuwa sio wanaume pekee wenye wivu wanaochukua hatua kama hiyo.

Welcome home: Or pehaps not? This photo was taken by a Reddit user in Washington State
Mke mwenye wivu anapochukua hatua


Mwezi Juni, mwanamke mmoja mjini Washington aliamua kumkaribisha mume wake kwa mtindo wa aina yake. Alichukua kitambaa na kuandika maneno yafuatayo: 'Welcome home, cheater (karibu nyumbani msaliti).' Kisha alikining’iniza kitambaa hicho nje ya nyumba yake.

Inasemekana kuwa mume huyo alieyekaribishwa kwa ujumbe huo alikuwa mwanajeshi ambaye alikuwa ametoka kwenye majukumu yake ya kikazi.


PICHA KWA HISANI YA GAZETI LA DAILYMAIL


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment