KIONGOZI MPYA AAPISHWA NCHINI MISRI

Adli Mansour, mkuu wa Mhakama Kuu ya Kikatiba nchini Misri ameapishwa kuwa rais wa mpito leo Julai 4, 2013.



Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Kikatiba nchini Misri, Adli Mansour, ameapishwa kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo.


“Ninaapa kuulinda mfumo wa jamhuri, na kuiheshimu katiba na sheria, na kulinda maslahi ya umma," Mansour aliyasema hayo leo wakati akila kiapo cha kushika wadhifa huo katika sherehe zilizofanyika katika jengo la Mahakama Kuu ya Kikatiba katika mji mkuu, Cairo.


Katika hotuba yake, kiongozi huyo aliyesimikwa na jeshi alilisifu na kulipongeza jeshi na vikosi vya polisi katika kuushughulikia mgogoro wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo.



Jana jumatano, Jenerali Abdel Fattah al-Sisi, mkuu wa majeshi, katika hotuba yake kwenye televisheni ya taifa, alitangaza kuondolewa madarakani Rais Mohamed Morsi.


Sisi alisema kuwa Morsi, ambaye alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia, "alishindwa kukidhi na kusikiliza matakwa ya wananchi."


Adli Mansour aliahidi kuongoza “nchi ya kisasa, kikatiba, uzalendo na ustawi."


Mansour aliendelea kusema kuwa chama cha Udugu wa Kiislamu (yaani Muslim Brotherhood) ni "chama cha kitaifa" na anakialika katika "ushiriki wa kujenga nchi."


Baada ya kufanya kazi kama naibu mkuu wa Mahakama Kuu ya Kikatiba tangu mwaka 1992, Mansour alichaguliwa kuwa mkuu wa mahakama hiyo mwezi Mei mwaka 2013 na kuanza kuutumikia wadhifa huo Julai 1.


Aidha, Mansour amesitisha matumizi ya katiba ya nchi na kusema kuwa uchaguzi mpya wa bunge utafanyika katika tarehe na muda utakaopangwa.


Kufuatia tangazo la Jenerali Sisi, polisi walianza kuwakamata wasaidizi muhimu wa rais na viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood.


Kuondolewa kwa Morsi kumekuja baada ya siku kadhaa za maandamano makubwa dhidi ya serikali yaliyofanyika nchi nzima.


Afisa mmoja mwandamizi wa jeshi la Misri amesema leo kuwa Morsi anashukiliwa na jeshi.


“(Morsi) anashikiliwa kwa ajili ya maandalizi ya mwisho," alisema ofisa huyo.



Morsi huwenda akakabiliwa na mashitaka rasmi kufuatia tuhuma zilizotolewa na wapinzania wake, afisa huyo alisema.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment