Kesi inayotaka Muungano waTanganyika na Zanzibar ufutwe imefunguliwa katika Mahakama Kuu yaZanzibar.
Kesi hiyo iliahirishwa jana Mahakama Kuu ya Vuga mjini hapa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi hadi Agosti 23, mwaka huu.
Mrajisi aliahirisha kesi hiyo iliyofunguliwa na watu 1,950 wa Unguja na Pemba kwa vile Jaji Mkuu waZanzibar, Omar Othman Makungu hakuwapo.
Kesi hiyo ya aina yake ambayo imepangwa kusikilizwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, inataka kubatilishwa kwa makubaliano ya muungano kati ya dola huru za Zanzibar na Tanganyika.
Wadai katika kesi hiyo wakiongozwa na mwanaharakati Rashid Salum Adiy, wanadai kuwa hakuna hati ya makubaliano ya muungano inayodaiwa kusainiwa Aprili 22, mwaka 1964 siku mbili kabla ya siku ya muungano, Aprili 26. Wafunguaji kesi hiyo wanadai kuwa, mambo kadhaa yanayohusu Muungano yalikuwa batili na kwa hiyo wanaitaka Mahakama Kuu ya Zanzibar itamke hivyo ili iruhusu kuzaliwa kwa dola huru ya Zanzibar yenye mamlaka kamili.
Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza, Mwanasheria Mkuu wa Muungano na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa.
CHANZO: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment