JOTO LIMEGHARIMU MAISHA YA WATU 760 UINGEREZA NDANI YA SIKU 9

 The hot weather has claimed the lives of up to 760 people in the UK between July 6 and 15.


Hali ya joto imegharimu maisha ya watu 760 nchini Uingereza kati ya Julai 6 na 15, hesabu rasmi zimeeleza.

Utafiti wa Gazeti la the Times uliofanywa na taasisi ya London School of Hygiene and Tropical Medicine (LSHTM) ulikadiria kuwa wimbi la joto nchini humo lilisababisha vifo vya baina ya watu 540 na 760 huku hali ya joto ikiwa haioneshi dalili za kupungua.

“Hatari ya vifo na maradhi mbalimbali inatupa wasiwasi mkubwa,” alisema  Profesa Virginia Murray, mkuu wa matukio ya dharura na kinga katika taasisi ya  Public Health England (PHE).

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, idadi hiyo inaweza kuongezeka mara dufu kwa kuwa hali ya joto inatarajiwa kuendelea kuwa juu angalau mpaka mwisho wa wiki ijayo.

Jana ndio siku iliyokuwa na joto zaidi kwa mwaka mzima, ikifikia kiwango cha zebaki 32.2C (90F).

Tahadhari ya kiafya ilitolewa mjini London na Kusini Mashariki, ikizitaka taasisi za afya kuwaangalia kwa ukaribu wazee, watoto na wale wenye maradhi sugu.

Joto kali linaweza kusababisha kiharusi joto, ambacho kinaweza kusababisha ubongo wa mtu kuharibika na hata kupoteza maisha.


CHANZO: Press Tv
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment