Maelfu ya watu wamehamishwa katika makazi yao katika mkoa mmoja magharibi mwa Ujerumani ambapo mto Elbe umefurika na kuvunja kuta zake.
Maeneo ya kusini na kaskazini mwa mji mkuu wa Hungaria tayari yapo chini ya maji, lakini eneo la katikati mwa mji, ikiwa ni pamoja na jengo la bunge na hoteli kadhaa jirani na ukingo wa mto, linaonekana kuepuka hatari ya moja kwa moja kwa sababu kuta zinazokinga mafuriko zilijengwa kwa urefu wa futi 30.5.
Kwa uchache vifo 21 vinavyohusiana na mafuriko hayo vimeripotiwa kutokea katika eneo la katikati mwa Ulaya, baada ya mito kama Danube, Elbe na Vlatava kufurika kufuatia wiki moja ya mvua nzito iliyonyesha na kusababisha hasara kubwa katikati na kusini mwa Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Austria, Slovakia na Hungary.
0 comments:
Post a Comment