Wanasiasa wanne kortini kwa uchoezi wa gesi Mtwara


Hassani Uledi (35), Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mtwara Mjini
Viongozi wanne wa vyama vya upinzani  mjini hapa, wamefikishwa katika Mahakama ya Makimu Mkazi  Mtwara na kusomewa mashtaka matatu ya kula njama, kufanya uchochezi na kuhamsha hisia mbaya kwa wakazi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washitakiwa hao ni Katani  Ahmed Katani (33) ambaye ni Mwenyekiti wa Vijana Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF); Hassani Uledi (35), Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mtwara Mjini; Hamza Licheta (51), Katibu Tanzania Labour Party (TLP) Mtwara Mjini na Saidi Kulaga (45), Katibu wa CUF wa Wilaya ya Mtwara.

Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri, Justine Sanga, aliwasomea mashitaka washitakiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi, Mussa Esanju, juzi.

Awali Sanga alidai kuwa katika kosa la kwanza, washitakiwa hao kwa pamoja walikutana mahali na muda usiojulikana na kula njama.

Mwendesha mashitaka hayo alidai kuwa katika kosa la pili Januari 16, mwaka huu, katika eneo la Bima Mjini Mtwara ,washitakiwa kwa pamoja walifanya kosa la  kutoa hotuba kwa wakazi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuleta chuki na kusababisha  kuharibu mali za umma na za watu binafsi.

Aidha, Sanga alidai kuwa katika shitaka la tatu Januari 16, mwaka huu, katika eneo la Bima Mjini hapa, washitakiwa  kwa pamoja wanadaiwa kuhamasisha hisia mbaya, kufanya mikutano ya kisiasa, kutoa maneno makali ya uchochezi na kusababisha kuamsha hisia za mbaya kwa wakazi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakili wa upande wa utetezi, Banana Biboze, aliiomba Mahakama hiyo kumwachia mteja wake Hassani Uledi, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu  cha Mjini Morogoro kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mitihani yake Juni 16, mwaka huu.

Hata hivyo, Hakimu Esanju alikataa kumwachia Uledi kwa dhamana pamoja na washitakiwa wengine kwa maelezo kuwa juendelea kukaa mahabusu ni kwa ajili ya  usalama wao na jamii kwa ujumla.

Licha ya kuwanyima washitakiwa hao dhamana, Hakimu Esanjupia alisema kuwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Dainess Lyimo, anayesikiliza kesi hiyo yupo safarini.

Washitakiwa kwa pamoja walikana mashitaka dhidi yao yao na kurudishwa rumande hadi na kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani Juni 13, mwaka huu.

Mei 22, mwaka huu ziliibuka vurugu za wananchi kupinga mradi wa kusafirisha gesi asilia kwa njia ya bomba kwenda Dar es Salaam wakitaka waelezwe namna watakavyonufaika.
 
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment