
Taasisi ya Usalama wa Taifa ya Marekani NSA imetengeneza chombo chenye nguvu cha kukusanya na kuzigawa kimakundi ya kiintelijensia nchi mbalimbali duniani.
Nyaraka za siri kuhusu ujasusi wa taasisi hiyo duniani na ambazo nakala yake moja imelifikia gazeti la The Guardian la nchini Uingereza zimefichua kuwa, chombo hicho kimepewa jina la "Jasusi Asiye na Mipaka" na kinatoa maelezo kuhusu hata ramani za nchi ambazo taasisi ya NSA imezikusanya kupitia kwenye mitandao ya kompyuta na simu.
Kwa mujibu wa Press TV, chombo hicho kinawapa uwezo watumiaji kuchagua nchi katika ramani na kuangalia taarifa zote zilizokusanywa na NSA dhidi ya nchi husika.
Nyaraka hizo zimefichua pia kuwa, katika muda wa siku 30 za mwezi Machi, Taasisi ya Usalama wa Ndani ya Marekani NSA ilikusanya vipande bilioni 97 vya taarifa za kiintelijensia kutoka mitandao ya kompyuta kote ulimwengu.
Bilioni 3 kati ya taarifa hizo za kijasusi zilikusanywa ndani ya Marekani kwenyewe. Nchi zilizolengwa zaidi kiujasusi na Marekani ni Iran ambapo taasisi hiyo ilikusanya vipande bilioni 14 vya taarifa za kijasusi kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi hicho cha siku 30.
Nchi nyingine ambazo Taasisi ya Usalama wa Ndani ya Marekani NSA ilikusanya taarifa za kijasusi katika kipindi hicho cha siku 30 za Mwezi Machi ni Pakistan, taarifa bilioni 13.5, Jordan, taarifa bilioni 12.7, Misri, taarifa bilioni 7.6, na India, taarifa bilioni 6.3 za kijasusi.
0 comments:
Post a Comment