![]() |
Polisi wakikabiliana na waandamanaji katika maandamano ya kupinga huduma mbovu za kijamii, unyanyasaji wa polisi na ufisadi wa serikali mjini Sao Paulo Juni 18, 2013
Serikali ya Brazili itatumia Kikosi cha Usalama wa Taifa vyenye silaha nzito katika miji mitano inayotarajiwa kutumika kwa mashindano ya kimataifa ya Soka katika juhudi za kudhibiti maandamano yanayoendelea katika nchi hiyo.
Tangazo hilo lililotolewa na Wizara ya Sheria linakuja baada ya siku moja ya makabiliano makali baina ya waandamanaji na na jeshi la polisi.
Kwa kawaida kikosi cha usalama wa taifa nchini Brazili hutumika kushughulikia migogoro nyeti ya kiusalama, kama vile maasi ya wafungwa au vurugu kubwa za magenge ya kihalifu.
Maandamano hayo yalizuka mapema mwezi huu kutokana na kupanda kwa gharama za usafiri wa umma na kuibua vuguvugu kubwa dhidi ya serikali, huku maelfu ya watu wakiandamana kuonesha hasira yao dhidi ya sera za serikali.
![]() |
Waandamanaji wakipita karibu na takataka zinazoungua katika maandamano ya kupinga huduma mbovu za kijamii, unyanyasaji wa polisi na ufisadi wa serikali mjini Sao Paulo Juni 18, 2013 |
Gharama kubwa za kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia nchini humo ni miongoni mwa masuala yaliyoibua maandamano hayo – waandamanaji wanasema kuwa bora pesa hizo zingetumika kutatua matatizo yanayoikabili jamii, badala ya kuzitumia kwenye tukio moja la kimichezo.
Jana Jumanne Rais wa Brazili, Dilma Rousseff alijaribu kutuliza joto la maandamano, akasema kuwa serikali yake inawajali raia na inataka kuyafanyia kazi manung’uniko ya waandamanaji. “Kiwango cha maandamano ya jana kinaonesha nguvu ya demokrasia yetu, nguvu ya sauti za waandamanaji na uzalendo wa wananchi wetu,” alisema katika hotuba iliyooneshwa katika vituo vya televisheni.
Aliendelea kulaani matukio ya ghasia na kuwataka waandamanaji waandamane kwa amani.
![]() |
Polisi wakijipanga wakati wa maandamano mjini Sao Paulo, Brazili, Juni 18, 2013 |
![]() |
Wanafunzi wakijaribu kuvunja mlango wa jengo la Ukumbi wa Jiji mjini Sao Paulo, Brazili Juni 18, 2013 |
![]() |
Wananchi wakiwa wamekusanyika kwenye medani maarufu ya September 7 mnamo Juni 18, 2013 mjini Belo Horizonte, katika jimbo la Minas Gerais |
![]() |
Wanafunzi wakishiriki maandamano katika eneo la Praca da Se, mjini Sao Paulo, Brazil Juni 18, 2013 |






0 comments:
Post a Comment