UTAFITI: JE, BANGI NI DAWA YA KANSA?
TAFITI mbalimbali zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika masuala ya tiba duniani, zimethibitisha kuwa mmea aina ya bangi unatibu ugonjwa wa kansa. Kwa mujibu wa wataalamu hao kutoka katika vyuo na taasisi zinazoheshimika duniani, Bangi ilitumika na inaweza kutumika kutengeneza mafuta ambayo hutibu magonjwa mbalimbali, ikiwemo kansa ya aina yoyote.
Mbali na kutibu kansa, wataalamu wanasema tayari mmea huo umeonyesha mafanikio katika kutibu magonjwa mengine yapatayo 200.
Miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na glaucoma, ambao husababisha upofu wa macho, husaidia kuondoa matatizo yanayojulikana kitabibu kama multiple sclerosis ambayo ni hali ambapo sehemu mbalimbali ndani ya mwili huwa ngumu.
"Bangi inazui matatizo ya kifafa kwa kiwango kikubwa sana,” alisisitiza Dk. Robert J. DeLorenzo, Profesa wa Chuo cha kitabibu ya Virginia, nchini Marekani.
Wanasayansi wa Uingereza nao waliwahi kuthibitisha kuwa bangi inaweza kusaidia kuzuia uvimbe unaosababishwa na kansa.
Kumekuwa na harakati za hapa na pale, hususani nchini Marekani na Uingereza za kutaka bangi ihalalishwe na itumike kama tiba.
Hali hiyo ambayo imekuwa ikizua mvutano ilisababisha wakati fulani Meya wa Jiji la New York kuunda tume ya wanasayansi kufanya utafiti kuona kama mmea huo una madhara ambayo yamekuwa yakitajwa, lakini matokeo ya uchunguzi huo yalibaini kwamba bangi ilikuwa kimea chenye manufaa mengi kuliko hata bidhaa kama pombe na sigara ambazo ni halali.
"Hakuna vifo vinavyotokana na matumizi ya bangi. Hakuna popote pale," alisema Dk. Lester Grinspoon, Profesa wa Chuo cha kitabibu cha Harvard.
"Sijawahi kusikia mtu kavuta kete kumi za bangi na akafa kwa ajili ya kuzidi vipimo, ila nimewahi kusikia na kuona mtu kameza vidoge vya malariquin ama madawa haya vya kisasa na kufa kwa ajili ya kuzidi vipimo vya dawa,” alisema Dk. Paul Hornby, mwana biolojia na mkemia (biochemist) pamoja na kuwa pathologia wa binadamu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini katika utafiti wa bangi.
Majarida mbalimbali yaliyochapishwa na wanasayansi kutoka katika vyuo vya kitabibu kama Harvard yanaeleza kwamba bangi ni muhimu katika afya ya binadamu, na inaweza kutibu matatizo ya binadamu kuliko madawa yanayopikwa kwenye maabara.
Marehemu Dk. Tod Mikuriya, aliyekuwa mtawala katika serikali ya Marekani katika utafiti wa bangi, alisema kwamba baada ya kushugulika na madawa mbalimbali karibia elfu kumi, bangi ilifanya vizuri zaidi katika magonjwa mbalimbali kama 200.
Pamoja na kwamba bangi hairuhusiwi kisheria hapa nchini, hata hivyo kwa miaka mingi katika nchi za wenzetu imekuwa ikitambulika na kutumika katika kutibu magonjwa fulani fulani.
Mbali na kuonekana kuwa na mafanikio na katika magonjwa hayo, pia nchini Marekani na nyingine za bara la Ulaya imekuwa ikitumiwa kuongeza nguvu katika tiba ya wagonjwa wa Ukimwi.
CHANZO: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment