DURU rasmi kutoka Somalia zinasema kuwa watu wapatao kumi wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika mlipuko wa Bomu lililotokea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.
Mashuhuda na maafisa mbalimbali wamesema kuwa baada ya mliupuko huo milio ya risasi ilisikika katika mji huo mkuu huo wa kibiashara na makao ya utawala wa nchi hiyo.
Shambuli hilo lilitokea umbali wa takriban mita 100 kutoka kwenye Ubalozi wa Uturuki.
Mnamo Aprili 2, mlipuko wa bomu ulitokea kwenye makao makuu ya benki ya Dahabshiil mjini Mogadishu, na kuzusha kizaazaa katika taasisi hiyo kubwa katika sekta ya kifedha.
Mlipuko huo ulitokea nje ya makao makuu ya benki hiyo saa chache baada ya wapiganaji wa al-Shabab kuiamuru kampuni hiyo kusimamisha shughuli zake katika maeneo wanayoyadhibiti.
Serikali dhaifu ya nchi hiyo imekuwa ikipambana na wapiganaji wa al-Shabab kwa miaka mitano sasa, na inaungwa mkono na vikosi imara vya Umoja wa Afrika kutoka Uganda, Burundi, na Djibouti.
0 comments:
Post a Comment