SYRIA YAPOKEA MAKOMBORA YA KINGA KUTOKA URUSI

Syrian President Bashar al-Assad
Rais wa Syria Bashar al-Assad



RAIS wa Syria, Bashar al-Assad amesema kuwa tayari Damascus imepokea awamu ya kwanza ya mitambo ya kisasa ya kuzuia makombora aina ya S-300 kutoka Urusi.



Katika mahojiano maalumu na kituo cha televisheni cha Al-Manar cha nchini Lebanon, Rais  Assad alisema kuwa awamu ya pili ya mitambo hiyo kutoka Urusi itawasili Syria hivi karibuni.



Aliongeza kuwa Syria itajibu mapigo dhidi ya uchokozi wowote utakaofanywa na Israeli dhidi ya nchi yake.




Mapema Mei 28, Urusi ilisema kuwa itaendelea na hatua yake ya kuipelekea Syria mitambo maalumu ya kuzuia makombora aina ya S-300, jambo lililoifanya Israeli kuja juu na kusema kuwa itachukua hatua ya kuzuia mitambo hiyo kupelekwa Damascus.



Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Walid al-Muallem baadaye alikaririwa akisema kuwa Syria itajibu "mara moja" uchokozi wowote utakaofanywa na ISraeli.


“Syria haitakubali uchokozi wowote wa Israeli upite bila kujibiwa. Majibu yatakuwa kwa kiwango kile kile cha uchokozi na kwa aina ya silaha hizo hizo zitakazokuwa zimetumiwa," alisema Waziri huyo wa mambo ya nje.



Kwa nyakati tofauti, Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu mnamo Mei 29, alisema kuwa Urusi inaweza kufikiria upya  kuhusu uwajibikaji wake katika utekelezaji wa vikwazo vya kuipelekea silaha serikali ya Syria, kufuatia uamuzi wa hivi karibuni wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kuhitimisha vikwazo vya silaha dhidi ya waasi wa Syria.



Urusi inasema kuwa mitambo hiyo inalenga kuzuia uvamizi na uingiliaji kati kutoka nje nchini Syria.



Syria imekumbwa na machafuko tangu Machi 2011 na kusababisha hasara na maafa makubwa kwa raia wa nchi hiyo.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment