Waokoaji wakimtoa katika kifusi mwanamke mmoja akiwa hai katika jengo lililoporomoka la Rana Plaza mjini Dhaka Mei 10, 2013. |
MWANAMKE mmoja ameokolewa kutoka kwenye kifusi cha jengo lililoprpomoka nchini Bangladesh siku kumi na saba baada ya zaidi ya wafanyakazi wa kiwanda kimoja cha nguo kupoteza maisha katika mkasa huo.
mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Reshma, alionekana baada ya kuwanyooshea mkono askari na waokoaji waliokuwa wakitafuta miili ya waathiriwa.
"Wakati tukiondosha kifusi, tuliita ili kuona kama kuna yeyote ambaye alikuwa hai,” afisa mmoja wa uokozi alikiambia kituo cha televesheni cha nchi hiyo, Somoy TV.
"Kisha tulimsikia akisema: 'niokoeni tafadhali, niokoeni tafadhali," afisa huyo aliongeza kusema.
Jengo la kiwanda kimoja cha kutengeneza nguo liliporomoka katika mji wa Savar jirani na mji mkuu wa nchi hiyo Dhaka Aprili 24, 2013. Takribani watu elfu moja walijeruhiwa vibaya sana, ikiwa ni pamoja na wale ambao viungo vyao vililazimika kukatwa ili kuwatoa katikati ya vifusi.
Vikosi vya usalama vinawashikilia watu kumi na mbili kuhusiana na janga hilo. Inaelezwa kuwa wahandisi na mmiliki wa kiwanda hicho waliwaagiza wafanya kazi waendelee kufanya kazi licha ya kujua fika kuwa kulikuwa na nyufa nyingi katika jengo hilo.
Wafanyakazi wamefanya maandamano wakitaka wahusika wapewe adhabu kali na kuwepo na sheria imara za usalama kazini.
0 comments:
Post a Comment