MTOTO WA MIAKA 2 AFARIKI DUNIA BAADA YA KIJIPIGA RISASI KICHWANI


A two-year-old has fatally shot himself in the US state of Texas with a gun belonging to his father.


MTOTO mdogo wa miaka miwili katika jimbo la kusini mwa Marekani la Texas amepoteza maisha baada ya kufanikiwa kuifikia silaha ya baba yake na kujipiga risasi kichwani.


Tukio hilo lilitokea Jumatano ya saa 2:46 usiku kwa majira ya  Marekani huko  Corsicana.

polisi wanasema kuwa mtoto huyo, aliyetambuliwa kama Kinsler Allen Davis, aliipata bunduki hiyo na kuifyatua wakati baba yake mwenye umri wa miaka 35 alipokuwa akitafuta kitu kabatini ndani ya chumba hicho hicho cha kulala.


Awali mtoto huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Eneo hilo ya Navarro, kabla hajasafirishwa kwenda kwenye Kituo cha Tiba cha Children's Medical Center mjini  Dallas, ambapo ilitangazwa kuwa alikuwa amefariki dunia.


Tukio hilo bado linachunguzwa. Tukio hili ni tukio jipya kabisa kutokea nchini Marekani likiwahusu watoto.

Tukio hili linafuatia tukio kama hilo lililotokea siku moja kabla ambapo mtoto wa miaka mitatu alifyatua risasi na kujiua baada ya kuichukua bunduki ya mjomba wake katika mji wa Tampa Bay.

Tarehe 4 Mei, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 6 alipigwa risasi kifuani na kaka yake huko Oakland Park.

Mnamo Aprili 30, mtoto wa miaka 5, alimpiga risasi dada yake wa miaka 2 kifuani wakati wakicheza nyumbani.


Mapema mwezi Aprili, mtoto wa miaka 4 huko New Jersey alichukua bunduki nyumbani kwao na kumuua rafiki yake wa miaka 6.


Mnamo Desemba 14, 2012, watoto 20 na wakubwa 6 walijeruhiwa vibaya sana na mtu aliyekuwa na silaha – ambaye baadaye yeye mwenyewe alijiua – katika shule ya awali ya Sandy Hook katika mji wa Newtown katika jimbo la Connecticut. Mapema siku hiyo, mshambuliaji huyo alimuua mama yake katika tukio la kabla ya hilo.


Kila mwaka, zaidi ya watu 30,000 hupigwa risasi na kuuawa nchini Marekani.

Wastani wa watu 87 hufariki dunia nchini humo kutokana na matumizi mabaya ya bunduki, huku watu 183 wakijeruhiwa kila siku.

Mwaka 2012 ulikuwa mwaka wa uwekaji wa kumbukumbu za mauzo ya bunduki nchini humo.

Hata hivyo, miito ya kuchukua hatua kali za udhibiti wa silaha inazidi kuongezeka, na kura za maoni zilizofanywa hivi karibuni nchini kote zinaonesha kuwa raia wengi wa Marekani wanaunga mkono uwepo wa udhibiti wa silaha.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment