MUUNGANO WA AFRIKA WAADHIMISHA MIAKA 50


A general view shows delegates attending the 50th African Union Aniversary Summit in Addis Ababa on May 25, 2013.
Wajumbe waliohudhuria Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa Mei 25, 2013.



Viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) wanakutana mjini Addis Ababa, Ethiopia kuadhimisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwa muungano wa bara hili.



Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa viongozi kutoka nchi 54 wanachama wa Umoja huo wanakutana kuadhimisha uhuru wa Afrika kutoka kwa utawala wa wakoloni waliolikalia bara hili kwa muda mrefu. 
 

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa AU na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn alisema kuwa mkutano huo utaangazia kuitengeneza Afrika isiyokuwa na umasikini na mizozo. 

"Siku hii ya kihistoria sio tu inaadhimishwa kwa ushindi mkubwa uliopatikana katika kukata kiuu ya muda mrefu ya uhuru, kujitegemea na umoja wa Afrika, bali pia ni mwanzo wa juhudi za pamoja za kuyafikia matarajio ya kijamii na kiuchumi ya Afrika,"  alisema Desalegn.

"Dhima kubwa kizazi cha sasa na cha baadaye ni kutengeneza bara lisilokuwa na umasikini na mizozo, bara ambalo wakazi wake watafurahia hadhi ya kipato cha kati," alisema. 

Ujumbe kutoka nchi mbalimbali, ukujumuisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, Rais wa Brazili, Dilma Rousseff na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry wanahudhuria tukio hilo. 

Maadhimisho hayo yatafuatiwa na mkutano wa siku mbili unaotarajiwa kuzungumzia mgogoro unaoendelea nchini Mali na kutafuta ufadhili wa kuusaidia umoja huo.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment