MAKOMBORA MAWILI YAUPIGA MJI MKUU WA LEBANON

People gather at the site of a rocket attack in Beirut, Lebanon, May 26, 2013.
Watu wakiwa wamekusanyika katika eneo lililopigwa na kombora mjini Beirut, Lebanon, Mei 26, 2013.



MAKOMBORA mawili yamepiga katika wilaya ya kusini ya Zahyieh katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.



Kwa mujibu wa duru za uslama nchini humo, watu kadhaa wamejeruhiwa katika tukio hilo lililotokea leo Jumapili. Baadhi ya magari na nyumba viliharibiwa.



Vyanzo vya usalama vinasema makombora aina ya 107-mm ndiyo yaliyotumika katika shambulizi hilo.  Mpaka sasa hakuna upande wowote uliodai kuhusika.



Kaimu Waziri wa mambo ya ndani Marwan Charbel, aliyetembelea eneo hilo alisema kuwa shambulizi hilo ni "kitendo cha hujuma."


“Makombora haya yalirushwa kutoka eneo maalumu, kusini mashariki mwa eneo la tukio," alisema.
 

“Ninaamini hiki ni kitendo cha hujuma,” Charbel alisema baada ya kuulizwa kuhusu jambo linaloweza kuwa limesababisha shambulizi hilo. “Ni matumaini yangu kuwa yanayotokea Syria hayatatokea Lebanon.” 

Tukio hili linakuja baada ya hivi karibuni kutokea makabiliano baina ya wapinzani na wale wanaoiunga mkono wa serikali ya Syria katika mji wa kaskazini wa Tripoli, Lebanon, lililosababisha vifo vya zaidi ya watu ishirini. 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment