Jumla ya watahiniwa 44,366 sawa na asilimia 87.85 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita mwaka 2013 wamefaulu, miongoni mwake wasichana wakiwa ni 14,622 sawa na asilimia 89.19 na wavulana 29,744 sawa na asilimia 87.21.
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 35,880 sawa na asilimia 83.74 wamefaulu katika madaraja la 1 hadi la 3 wakiwemo wasichana 12,108 sawa na asilimia 87.30 na wavulana 23,772 sawa na asilimia 82.04.
Jumla ya watahiniwa 52,513 waliandikishwa kufanya mtihanai wa kidato cha sita mwaka huu wakiwemo wasichana 16,934 sawa na asilimia 32.25 na wavulana 35,579 sawa na asilimia 67.75.
Kati ya watahiniwa 52,513 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita February 2013 watahiniwa 50,611 sawa na asilimia 96.38 walifanya mtihani na watahiniwa 1,902 sawa na asilimia 3.62 hawakufanya mtihani.
Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA Dk.Charles Msonde akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari anasema pamoja na ufaulu kuongezeka lakini Baraza hilo limezuia matokeo ya baadhi ya watahiniwa kwa sababu mbalimbali ambao wengine wamepewa nafasi ya kurudia mtihani.
Kuhusiana na suala la udanganyifu amesema umepungua na kwa wachache waliobainika kufanya udanganyifu tayari wamefutiwa matokeo ya mtihani.
Shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa 30 za zaidi ni pamoja na Marian Girls ya Pwani, Mzumbe Sekondary ya Morogoro, Feza boys ya Dar Es Salaam, Ilboru Sekondary pamoja na Kisimiri zote za Arusha.
Shule 10 za mwisho katika kundi la shule zenye watahiniwa 30 na zaidi ni pamoja na Pemba Islamic College ya Pemba, Mazizini Sekondary ya Unguja, Bariadi ya Simiyu, Hamanmni pamoja na Dunga zote za Unguja.
Shule 10 bora katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 30 ni Palloti Girls ya Singida, St.James Seminary, Parane na Sangiti zote za Kilimanjaro pamoja na Itamba Sekondari ya Njombe.
Aidha shule 10 za mwisho katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 30 ni Mbarali Preparatory School na Philter Federal zote za Unguja, St.Marys na Mzizima zote za Dar Es Salaam, Hijra Seminary ya Dodoma pamoja na Tweyambe ya mkoani Kagera.
0 comments:
Post a Comment