Rais Bashir wa Sudan akihutubia mkutano wa vyama vya kisiasa Afrika, Khartoum Aprili 27 2013 |
Wawakilishi wa vyama 35 vya kisiasa barani Afrika vyenye uwakilishi bungeni wamekutana katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum kwa lengo la kuanzisha jukwaa la kuimarisha umoja wa nchi za Afrika.
Akihutubia kikao hicho cha Baraza la Vyama vya Kisiasa Afrika siku ya Jumamosi, Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesema kikao hicho ni hatua ya kwanza ya kimsingi ya kuleta umoja kamili barani Afrika.
Rais Bashir amesema pamoja na kuwa bara la Afrika lina historia iliyojaa utajiri na idadi ya watu wanaozidi bilioni moja, lakini bado Waafrika hawana uwakilishi unaofaa katika vikao vya kimataifa. Mshauri wa Rais wa Sudan Nafie Ali Nafie amesema kikao hicho kinalenga kuleta umoja na kuunda taasisi ya vyama vyote vya kisiasa Afrika. Kamishna wa Masuala ya Kisiasa katika Umoja wa Afrika Bi. Aisha Abdullahi pia alihudhuria sherehe za ufunguzi wa kikao hicho.
0 comments:
Post a Comment